وكالة أهل البيت (ع) للأنباء

المصدر : Parstoday
الأربعاء

٣١ مايو ٢٠٢٣

١:٥٦:١٤ م
1370143

Wanasiasa wa Misri wakaribisha kustawishwa uhusiano wa Tehran na Cairo

Wanasiasa na viongozi wa Misri wamekaribisha kwa mikono miwili juhudi za kuhuishwa na kurejeshwa uhusiano wa Iran na Misri.

Wakizungumza na gazeti la al-Sharq al-Awsat, viongozi hao wamesema kuwa, Cairo inakaribisha kwa mikono miwili ishara chanya zilizoonyeshwa na Iran za kuwa tayari kustawishwa uhusiano wa pande mbili.

Nabil Fahmi, Waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni wa Misri sambamba na kubainisha kwamba, katika miaka iliyopita kumekuweko na mawasiliano baina ya viongozi wa Misri na Iran ameeleza kuwa, viongozi wa Tehran na Cairo wamefanya mazungumzo kuhusiana na umuhimu wa kustawishwa uhusiano baina ya mataifa yao na wameunga mkono hilo.

Hivi majuzi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema Iran inakaribisha azma ya kufufuliwa uhusiano wake na Misri.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema hayo katika mazungumzo yake na Sultan Haitham bin Tariq Aal Saeed wa Oman na kuongeza kuwa, "Tunakaribisha msimamo huu, na hatuoni tatizo katika (kufikiwa) hilo." 

Hivi majuzi pia, maafisa wawili wa serikali ya Misri waliliambia gazeti la Imarati la The National kwamba, uhusiano wa Tehran na Cairo ni miongoni mwa mambo muhimu yaliyojadiliwa katika mazungumzo ya Sultan wa Oman na Rais Abdul-Fattah al-Sisi na kwa muktadha huo kuna uwezekano katika miezi michache ijayo, Iran na Misri zikabadilishana mabalozi.

uhusiano wa kidiplomasia wa pande mbili ulikatwa baada ya Iran kulalamikia mkataba wa Cairo-Tel-Aviv mashuhuri kwa jina la mkataba wa amani wa Camp David. 

342/